KWANINI WANAUME HUCHEPUKA?
- Maana
- Sababu
- Madhara
- Matibabu
- Hitimisho
Kuchepuka ni nini?
Maana halisi ya kuchepuka ni kupita njia ya pembeni badala ya njia kuu.
Kuchepuka katika ndoa ni nini?
Kuchepuka katika ndoa ni kuwa mpenzi wa pembeni kwa siri. Mtu ambaye hana mke hawezi kuambia anachepuka kwa sababu ile njia kuu haipo.
Kwanini wanaume huchepuka?
Sababu za kumfanya mwanaume kuchepuka ni nyingi sana lakini pia nyingi katika hizo huzuilika kama endapo baadhi ya mambo yakifanyiwa kazi.
v Kumsahau Muumba
Kuzini ni dhambi katika dhambi mbaya zaidi duniani. Kila imani ya dini inaamini hivyo. Na laiti mwanadamu angejua uzito wa dhambi wala asingeisogelea kamwe.
Zinaa ni uchafu. Panapo majaaliwa siku moja nitakuja na mada kukueleza kwanini zinaa ni uchafu?
v Maumbile
Iko wazi kuwa mwanaume ni tofauti na mwanamke kimaumbile, tamaa za kimwili, hisia na hata ujasiri.
Hii ni asili kwa jamii zote za viumbe wenye jinsia ya kike na kiume kuanzia wanadamu, wanyama, majini, wadudu na kadhalika.
Hili liko wazi na linafahamika. Hata katika dini ya Uislamu kwa kuliona hili wakaweka chaguo la kuoa mwnamke zaidi ya mmoja. Hii ni kwa sababu ya asili ya mwanaume.
v Kero majumbani
Visirani vya mwanamke kwa mwanaume wake. Mwanamke ameumbwa kuchukia, kufurahi na kukereka wakati mwingine bila sababu yoyote au kwa sababu zisizokuwa na msingi.
Sababu hizi zinaweza kumpelekea kumnyima mume wake haki yake ya ndoa. Kama mwanaume asipokuwa makini na hali hiyo anajikuta anaangukia katika dimbwi la kuchepuka.
v Mabadiliko ya maumbile ya mwanamke
Mwanamke ana likizo nyingi sana ambazo hawezi kushiriki mapenzi na mume wake. Miongoni mwazo ni Hedhi, Mimba kubwa, uzazi na kadhalika.
Baadhi ya wanawake likizo hizo huchukua kipindi kirefu na kumpelekea mwanaume kuanza kutafuta njia mbadala (mchepuko)
v Kazi kupitiliza
Baadhi ya wanawake wanafanya kazi sehemu mbali mbali ikiwemo maofisini, mashambani na kazi binafsi (Hii sio mbaya).
Mbaya zaidi ni pale mwanamke anapokuwa na majukumu kupitiliza na kukosa hata muda wa kupumzika na mume wake au kuchoka na kushindwa kumhudumia bwana.
v Changamoto za mazingira
Naam, mazingira yanamchango kiasi fulani katika kupelekea mwanaume kuchepuka. Mazingira ya makazini wanawake huvaa mavazi ya ajabu na mitego mingi. Mazingira ya safarini, majumbani tunamoishi na sehemu nyingine nyingi.
Mwanaume ni kumbe dhaifu sana kwa mwanamke hasa panapotokea mitego ya makusudi.
v Uadui wa wanawake
Kama nilivosema hapo juu kuwa mwanaume ni dhaifu kwa mwanamke. Hii inaweza kuwa fursa kwa mwanamke asiye na maadili kumkomesha mwanamke mwenzake kwa kumchukulia mume wake.
Huu ni uadui baina ya wanawake na wanaamini njia ya kumkomesha mwanaumke mwenzake ni kumchukulia bwana wake. Waliobahatika kuishi mikoa ya Pwani wanaelewa hili.
v Umbali
Mume na mke kuwa mbali mbali kwa muda mrefu nayo hupekea mwanaume kuingia katika majaribu haya ili kukidhi mahitaji yake ya kimwili.
v Mazoea na kukosa ubunifu
Katika ndoa au mahusiano ya muda mrefu inafika kipindi mnazoeana kuonana kuwa hakuna maajabu.
Mapenzi ni ubunifu kila siku, kukaririka kwa baadhi ya mambo kunaweza kumfanya mwanando mmoja kwenda nnje kutafuta mbinu mpya au jambo jipya ambalo amelisikia na kwa mke wake hakuna jambo hilo.
v Kuenea kwa teknolojia
Ujinga ni kuamini kwa mwanaume kuwa na michepuko mingi basi ndiyo uanaume. Hii sio sahihi
Kuenea kwa teknolojia hasa mitandao ya kijamii imekuwa ni chanzo kikubwa sana cha kuhamasisha watu kuwa na wanawake wengi bila kujali na kujitutumua mbele ya wengine. ‘SIO UJANJA’
v Matumizi mabaya ya madawa
Hapa namaanisha dawa zinazo sadikika kuongeza nguvu za kiume. Kuna muda unaweza kunywa madawa yako unafika nyumbani mke hayuko sawa kwa namna yoyote ile na ndio umeshajimaliza unahisi nini kitatokea kama sio kutokea mlango wa nyuma?
v Kurithi
Ushenzi pia hurithiwa, tabia pia hurithiwa na maumbile pia.
Huenda ukoo wa mtu asili yao ni ushenzi kama huo, na hii pia ni sababu kubwa za mwanaume kuwa na michepuko mingi. ‘NGUMU KUMEZA’
v Tamaa
Umewahi kusikia neon ‘SHUGA MAMY’?
Basi kama hujawahi kusikia, hawa ni wanawake wakubwa (mimama) ambao hupenda sana kutembea na vijana (mabarobaro)
Yuko tayari kukupa chochote ili tu afanyeu chafu na wewe maadamu ameona umemfaa. Hajali una mke au laa
Kwa kijana ambaye ana tama aidha ya pesa, umaarufu, gari na kadhalika ni rahisi kuingia katika tego hili. ‘VIJANA WA MJINI WANANIELEWA’
v Makundi
Rafiki zako na jamaa zako wa karibu kila mtu ana michepuko kadhaa, wanakuona bwege kubaki na mke wako. Wanaamua kukutafutia kimwana mrembo wa kukutuliza, nawe unakubali unaingia laini. Hapo wanakusifu na kukuona sasa ni mjanja. ‘HAYA NDIO MAKUNDI’
Sababu za mwanaume kuwa na michepuko ni nyingi sana, lakini hizo ni chache tu. Unaweza kuniongezea nyingine hapo chini ya makala hii sehemu ya COMMENT
Madhara ya michepuko ni makubwa sana na nadhani unayafahamu. Labda nikukumbushe tu kwa kuyaorodhesha kwa haraka haraka
a. Maradhi
b. Vifo
c. Kuvunjika kwa ndoa
d. Watoto wa mtaani
e. Kupoteza kazi
f. Kufilisika kwa biashara
g. Umasikini
h. Kupoteza marafiki
i. Kupoteza amani
j. Kupata adhabu kali ya Mungu kesho akhera / Mbinguni
Njia za kuepuka / kuacha michepuko
v Lishike neno la Muumba wako
Zitambue adhabu za Mungu, omba sana, Sali sana, fanya ibada nyingine ambazo zitakufanya kumkumbuka Mungu zaidi.
Tembelea wagonjwa, hudhuria misiba, zuru makaburi na kadhalika
IPE NYONGO DUNIA, USIIENDEKEZE
v Ogopa fedheha na magonjwa
Tazama jinsi wagonjwa wa Ukimwi wanavyofanyaika sasa. Jua kwamba ukiendekeza zinaa huenda nawe ukawa kama wao (Japo sio wote waliopata ukimwi kwa zinaa)
Fikiria waliofadhaika kwa kufumaniwa na wake za watu na kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Fikiria kuhusiana na waliofungwa kwa sababu ya kuwapa mimba watoto wa shule.
TAFAKARI TAFAKURI HIZO NA UTAPATA MAZINGATIO
v Kuwa mwanaume (Gentleman)
Mwanaume mtanashati hawezi kuvua nguo zake kwa kila mwanamke. Mwanaume mtanashati husifika kwa tabia nzuri na heshima. Mwanaume mtanashati sio mali ya UMMA, ni mali ya mke wake tu / wake zake.
v Usikubali kununulika kwa gharama yoyote
Waswahili walishasema ‘Tamaa mbele mauti nyuma’
v Mpende mke wako
Mpende, mthamini, muheshimu mke wako. Kamwe huwezi kumgeuka kwa kumzunguka na wanawake wengine wasio mali yako.
v Puuza
Umepita mitaani, kazini, barabarani ukaona wanawake wenye maumbile mazuri huenda kuliko uliyenaye. Puuza na ione ni hali ya kawaida na yatapita tu.
Waone kama umeona moto.
v Epuka marafiki waovu
v Omba msaada kutoka kwa Mungu
Hakuna mwanaume timamu anaweza kuruka viunzi vya mitihani ya wanawake ila ni kwa msaada wa Mungu pekee.
Maombi iwe ni silaha yako kila wakati.
NAKUAGA KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Post a Comment